Sponsor


Breaking News

Sunday, June 11, 2017

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge yaanza Ufaransa

Raia wa Ufaransa leo hii wameanza kupiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge nchini humo, huku chama chenye mwaka mmoja tangu kuundwa kwake cha mrengo wa wastani cha rais aliechaguliwa hivi karibuni Emmanuel Macron kikitabiriwa kushinda wingi wa viti bungeni. Uchunguzi wa mwisho wa maoni uliofanyika mara ya mwisho unamweka Macron na chama chake cha "The Republic on the Move," LREM katika asilimia 29 hadi 31.3 katika duru hii. Mpinzani wake wa karibu chama cha mrengo wa kati kulia "Les Republicains" kinaweza kuibuka na asilimia 19 hadi 23. Wakati huohuo chama cha kisoshalisti cha mtangulizi wa Macron, Francois Hollande,kipo katika mashaka ya kuporomoka. Macron ana matumani ya kuibuka na wabunge 577 katika bunge la taifa ili aweze kuidhinisha serikali yake, inayoongozwa na Waziri Mkuu Edouard Philippe.
default
Read more ...

Marekani yafuta kazi madera taxi za Ube

Kampuni ya kimarekani yenye kutoa huduma ya taxi, Uber, imearifu kwamba imewafuta kazi wafanyakazi wake 20 baada ya uchunguzi dhidi ya malalamiko ya unyanyasaji wa kijinsia na mambo mengine.
BBC inafahamu kwamba, baadhi ya waliofutwa ni wafanyakazi wa vyeo vya juu.
Timua hiyo inafuatia msururu wa kashfa kwa kampuni hiyo ya Uber ambayo imeibua maswali kuhusu mfumo wa biashara yake, The sackings follow a series of scandals.
Malalamiko mingi yametokwa kwa wafanyakazi katika ofisi zake za San Francisco. Uber imesema laini ya simu ya faragha kwa watumizi wake, iliyoanzishwa mwezi February, itaendelea kutumika ili kubadilisha jinsi watu wanavyofanya kazi katika shirika hilo.
Marekani
Read more ...

Mabaki ya binadamu 'wa kwanza' yapatikana Morocco

Uchunguzi umebainisha kuwa dhana ya kuwa asili ya binadamu wa kwanza ni kutoka Afrika ya Mashariki zaidi ya miaka laki mbili iliyopita sio kweli.
Visukuku vya binadamu watano wa mapema imepatikana Kaskazini mwa Afrika na inaonyesha binadamu wa kwanza aliishi miaka 100,000 zaidi ya vile ilivyodhaniwa.
Prof Jean-Jacques Hublin, kutoka Leipzig, Ujerumani, anasema kuwa ugunduzi huu unaweza "kuandika upya vitabu vya kiada" kuhusu kuibuka kwetu .
"Sio hadithi ya hayo kutokea kwa njia ya haraka katika 'shamba la Edeni' mahali fulani barani Afrika. Ilikuwa ni maendeleo ya taratibu. Kwa hiyo kama kulikuwa na bustani ya Edeni, ilikuwa ni kote kote Afrika.
Prof Hublin alikuwa akiongea katika mkutano wa wanahabari katika chuo kimoja mjini Paris, ambako aliwaonyesha waandishi kisukuku ambacho timu yake ilichimbua katika eneo la Jebel Irhoud, Morocco. Sampuli hiyo ni ya na fuvu, meno na mifupa mirefu.
Mabaki yaliyopatikana katika eneo hilo hapo awali yalisemekana kuwa na miaka elfu 40. Lakini Prof Hubli alikuwa na tashwishi na kwa muda mrefu aliendelea kufanya utafiti katika eneo hilo la Jebel Irhoud na miaka 10 baadaye, anawasilisha ushahidi mpya unaoelezea hadithi tofauti.
Mabaki hii ya sasa inadaiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 300,000 na 350,000 miaka. Na fuvu yake ni ya aina karibu sawa na ya binadamu wa kisasa.
Hadi sasa, mabaki ya binadamu wa kwanza yalikuwa kutoka Ethiopia (kutoka tovuti inayojulikana kama Omo Kibish) , Afrika mashariki na walidaiwa kuwa na umri wa takribani miaka 195,000.
Kabla ya watu wa aina yetu, kulikuwa na aina nyingi tofauti ya binadamu, na kila alikuwa na uwezo na udhaifu tofauti. Na hawa aina mbalimbali ya binadamu, kama vile wanyama wengine, waliendelea kubadili muonekano wao hatua kwa hatua.
Jebel Irhoud inafanana na sehemu kadhaa za kihistoria barani Afrika ambayo ina miaka 300,000. Maeneohaya yana zana sawa na pia ushahidi wa matumizi ya moto.

Ujenzi wa kwanza wa kisukuku cha awali zaidi cha binadamu kutoka Jebel Irhoud (Morocco) kulingana na nakala za tomografia.

Read more ...

Iran yasafirisha chakula kuenda taifa lililotengwa la Qatar

Iran imetuma ndege tano zilizosheheni chakula kuenda nchini Qatar, ambayo inakumbwa na uhaba wa chakula baada ya kutengwa na nchi zingine za kiarabu.
Mataifa kadha yakiwemo hasimu mkubwa wa Iran, Saudi Arabia, wiki iliyopita yalikata uhusiano na Qatar baada ya kuishutmu kwa kufadhili ugaidi.
Mpaka na Saudi Arabia ambapo asilimia 40 ya chakula cha Qatar hupitia umefungwa.
Raia wa Qatar wamemrishwa kuondoka kutoka mataifa hayo lakini Qatar imesema kuwa haitafanya hivyo.
Hajulikani ikiwa chakula hicho ni cha msaada au ni cha kuuzwa.
Shirika la ndege la Iran liliandika katika mtandao wa twitter, wakati chakula hicho kikijazwa kwenye ndege nchini Iran.
Wadadasi wanasema kuwa uhusiano mzuri kati ya Qatar na Iran ni moja ya sababu zilizochangia mzozo huo
Iran Air posted a tweet of a shipment being loaded at Shiraz airport
Read more ...

Saturday, April 29, 2017

Facebook kuongezwa masomoni chuo kikuu India

Kuandika ujumbe na kupakia picha na video limekuwa jambo la kawaida kwa karibu watu 1.8 bilioni wanaotumia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Ingawa ujumbe wako wa siasa au salama za heri, pongezi au rambirambi unaweza kupendwa na wenzako, si wengi wanaoweka kuchukulia ujumbe huo kuwa fasihi au kazi ya sanaa.
Lakini sasa Chuo Kikuu cha Delhi (DU) kimechukua msimamo tofauti.
Kinataka kujumuisha kuandika ujumbe wa Facebook kuwa sehemu ya mtalaa wake wa somo la Kiingereza.
Wanafunzi watakuwa wakifunzwa pia jinsi ya kuandika blogu au barua kuu ya kujitambulisha wakati wa kuwasilisha maombi ya kazi.
DU ni miongoni mwa vyuo vikuu bora zaidi nchini India.

Miongoni mwa waliowahi kusomea katika chuo kikuu hicho ni waziri mkuu Narendra Modi na kiongozi wa Burma na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Aung San Suu Kyi.
Mambo hayo yamejumuishwa kwenye mswada wa mtalaa wa Kiingereza ambao unatathminiwa na maprofesa wa DU.
Prof Christel Devadawson, mkuu wa kitivo cha lugha ya Kiingereza aktika chuo kikuu hicho, aliambia BBC kwamba ujumbe kwenye Facebook utatumiwa kama sehemu ya Kozi ya Kuimarisha Ujuzi - ambayo ni sehemu ya somo inayotumiwa kuwapa wanafunzi maarifa na ujuzi wa kuwawezesha kufaa maeneo ya kazi.
Gazeti la Hindustan Times linasema nchini India, mitandao ya kijamii inaweza kumzolea umaarufu mkubwa mwandishi chipukizi au msanii na kumuwezesha kufikia watu wengi au hapa kupata matbaa ya kuchapisha kazi zake.
 Facebook kwenye simu
Read more ...

Mume na mke waliooana miaka 69 wafariki pamoja Marekani

Wanandoa wawili katika jimbo la Illinois, waliokuwa wameoana kwa miaka 69, walifariki wakiwa wameachana kwa saa moja pekee, jamaa zao waliambia vyombo vya habari Marekani.
Isaac Vatkin, 91, alikuwa amemshika mkono mkewe Teresa, 89, alipofariki kutokana na ugonjwa wa Alzheimer Jumamosi, gazeti la Daily Herald.
Isaac alifariki dakika 40 baadaye.
Jamaa zao walisema walifarijiwa kwamba wawili hao walikuwa pamoja hadi mwisho.
"Hungelipenda kuwaona wakituacha,"
"Upendo wao kwa kila mmoja ulikuwa mkubwa sana, mmoja wao hangeweza kuishi bila mwenzake," binti yao Clara Gesklin alisema wakati wa mazishi yao.
"Walipendana sana, hadi mwisho. Hadi sekunde ya mwisho," alisema Rabbi Barry Schechter, aliyeongoza ibada ya wafu katika eneo la Arlington Heights, viungani mwa mji wa Chicago.
Wafanyakazi katika hospitali ya Highland Park wamesema waliwapata Bwana na Bi Vatkin wakiwa wanatatizika kupumua Jumamosi na wakaamua kuweka vitanda vyao vikiwa vimekaribianaalisema mjukuu William Vatkin, "lakini hungetaka zaidi ya hilo."
 Wawili hao walikuwa wameoana kwa miaka 69
Read more ...

Mtoto aliyezaliwa na miguu 3 afanyiwa upasuaji Australia

Mtoto mmoja nchini Bangladesh aliyezaliwa akiwa na miguu mitatu amefanyiwa upasuaji nchini Australia na sasa anarudishwa nyumbani
Choity Khatun ambaye ana miaka mitatu alizaliwa na ulemavu huo ambapo mguu huo ulikuwa umemea katika mfupa wake wa kiuno.
Wapasuaji wa Australia walitumia mwezi mmoja wakifanya kazi ya kuuondoa mguu huo na kurekebisha eneo lake la mfupa wa kiunoni.
Mtoto huyo alipelekwa Australia kutoka kijijini kwao huko Bangladesh na shirika moja la hisani Children first Foundation.
Daktari Chris Kimber ,kiongozi wa upasuaji katika hospitali ya Monash huko Victoria alisema kuwa kesi ya Choite ilikuwa isio ya kawaida na kwamba upasuaji huo ulikuwa mgumu.Upasuaji hutegemea mtu anayefanyiwa na lazima utumie muda mwingi kuchanganua ni nini kilichopo na baadaye upange mpango unaoshirikisha hayo yote'', aliambia kituo cha habari cha Australia Broadcasting Cooperation.
Kundi hilo la madaktari wa Australia pia lilikuwa limefanya majadiliano kuhusu upasuaji huo
Lilijadiliana iwapo upasuaji huo ulihitajika na kwamba ungemfaidi kabla ya mtoto huyo kupelekwa Australia.
Mtoto wa miaka mitatu aliyezaliwa na miguu mitatu
Read more ...

Kombora jingine la Korea Kaskazini lafeli majaribio

Rais wa Marekani Donald Trump ameishtumu Korea kaskazini kwamba imeikosea heshima China, mshirika wake mkuu, kwa kufyatua kombora la tatu katika kipindi cha mwezi mmoja.
Kwenye ujumbe wa Twitter, bwana Trump amemsifu rais wa Uchina, Xi Jinping.
Maafisa wa Marekani na Korea Kusini wanasema jaribio hilo lilitibuka, kwani kombora hilo lilianguka punde tu baada ya kupaa angani.
katika mkutano wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, Rex Tillerson, ameonya kwamba huenda kukaibuka majanga mabaya sana iwapo miradi ya Kim Jong Un ya kutengeneza zana za kinyuklia na makombora ya masafa marefu hiatositishwa.
Maafisa wa Marekani wanasema kombora hilo lilipaa angani kwa sekunde kadhaa kabla ya kuanguka.Korea kaskazni
Read more ...

Sunday, April 16, 2017

Ombi la kutaka kuhalalisha bangi Kenya laungwa mkono

Zaidi ya Wakenya 1,400 wanaunga mkono ombi la kutaka kuidhinishwa kwa matumizi ya mmea wa bangi baada anayewasilisha hoja hiyo kuwawasilisha ombi lake mbele ya bunge la seneti.
Iwapo ombi hilo la mtafiti Gwada Ogot litaidhinishwa haitakuwa haramu kupanda ama hata kuuza bangi nchini Kenya.
Gwada Ogot anasema kwamba matumizi ya kiafya pamoja na utumizi wa mmea huo viwandani unaojulikana kwa jina la sayansi kama Cannabis sativa una faida nyingi.
Anasema kuwa matumizi ya mmea huo yataimarisha hali ya uchumi.
Sheria ya Kenya inapiga marufuku utumizi wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.
Ogot anaomba bangi kuondolewa miongoni mwa orodha ya vitu haramu na kutaka sheria mpya kuanzishwa ili kuweka bodi simamizi ya utumizi wa mmea huo.

Ombi la kutaka bangi kuhalalaishwa kenya laungwa mkono

Read more ...

Mtoto wa miaka 8 aendesha gari kununua chakula duka la McDonald's

Mtoto mmoja mvulana mwenye umri wa miaka minane katika jimbo la Ohio, aliendesha gari akiwa na dadake mdogo hadi duka la McDolad's baada ya kujifunza kuendesha gari kupitia mtandao wa YouTube.
Jarida na Morning Journal la Ohio lilisema kuwa polisi walipigiwa simu kutoka kwa wenyeji kuhusu mtoto ambaye alikuwa akindesha gari mjini.
Wafanyakazi katika mkahawa wa McDolad's walidhani kuwa ulikuwa ni mchezo wa kuigiza wakati mtoto huyo alisimamisha gari kwenye dirisha kununua chakula.
Mtoto huyo alifuata shera zote za barabara, mtu mmoja aliyeshuhudia alisema.
"Hakugonga chochote njiani, polisi Jacob Koeher kutoka kijiji cha East Palestine alisema

Mtoto wa miaka 8 aendesha gari kununua chakula

Read more ...

Sylvester Stallone anaishitaki studio ya filamu ya Warner Bros kwa kukosa kumpa kiwango cha pesa walichokubaliana kama faida, kutoka filamu ya mwaka 1993 ya Demolition Man.

Stallone anasema filamu hiyo ilitengeneza dola milioni 125 kwenye box office na kulingana na mkataba wake na studio hiyo, anastahili kupewa asilimia 15 ya pesa hizo.
Stallone anasema "studio za Motion Picture wanajulikana kuwa walafi" na warner Bros "walizuia fedha zangu" kwa miaka "bila ya sababu yoyote ile."
Warner Bros bado haijasema lolote kuhusu hatua hii ya kisheria.
Makaratasi ya kisheria ya Stallone yanaonyesha kuwa wawakilishi wake walijadili swala hilo na Warner Bros mwaka wa 2014 lakini waliarifiwa kuwa kampuni hiyo ya filamu haiwezi kumlipa Stallone chochote kwa sababu filamu ya Demolition Man ilipoteza dola milioni 66.9.
Stallone alihoji uamuzi huu na mwezi Aprili mwaka 2015 kampuni hiyo ilimtumia Stallone hundi ya dola milioni 2.8.
Kesi hii imefikishwa mbele ya mahakama ya Los Angeles na Stallone anataka ukaguzi wa pesa zote kutoka kwa filamu hiyo ufanywe.
Stallone aliigiza katika filamu yaSylvester Stallone Demolition Man pamoja na Wesley Snipes.
Read more ...
Makumi ya maelfu ya watu kote katika Marekani wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mbalimbali wakitaka Rais Donald Trump, kutangaza kodi aliyolipa kwa Serikali, jambo ambalo yeye binafsi amekataa kufanya.
Waandamanaji wengine walibeba sanamu kubwa za kuku, wakimaanisha kuwa Rais ni mwoga na amekataa kutoa takwimu za kodi yake.
Karibu watu 14 wametiwa mbaroni katika Berkeley, katika Carlifornia ambako wafuasi wa Rais Trump na wapinzani wake walikabiliana.
ngawa hakuna sheria inamlazimu Bwana Trump kutangaza kodi yake, Marais wote wa Marekani wamekuwa wakifanya hivyo kwa muda wa miongo minne iliyopita.
Maandamano hayo yalipangwa kwenda sambamba na siku ya mwisho ya raia kuwasilisha takwimu zao za kodi.
Maelfu waandamana kutaka Trump kutangaza kodi aliyolipa kwa serikali
Read more ...
Korea Kaskazini imejaribu kufyatua kombora moja lakini likakosa kupaa angani, siku moja tu baada ya kuonya Marekani kuwa haiogopi vitisho vyake vya kivita.
Jeshi la Marekani lilisema kuwa kombora hilo lililipuka sekunde chache baada ya kufyatuliwa katika ufuo wa Mashariki wa Korea Kaskazini.
Afisa mmoja wa Marekani alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa kombora hilo halikuwa la masafa marefu linaloweza kutoka bara moja hadi jingine.
Rais Trump alifahamishwa juu ya jaribio hilo lililofanywa masaa machache kabla ya Makamu wa Rais Mike Pence kuwasili Korea Kusini, kwa mashauri kuhusiana na Pyongyang na mipango yake ya makombora ya kinyukilia.
Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa siku moja baada ya maonyesho ya zana na kijeshi
Read more ...
Designed By Published.. Blogger Templates