Korea Kaskazini imejaribu kufyatua 
kombora moja lakini likakosa kupaa angani, siku moja tu baada ya kuonya 
Marekani kuwa haiogopi vitisho vyake vya kivita.
Jeshi la Marekani
 lilisema kuwa kombora hilo lililipuka sekunde chache baada ya 
kufyatuliwa katika ufuo wa Mashariki wa Korea Kaskazini.Afisa mmoja wa Marekani alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa kombora hilo halikuwa la masafa marefu linaloweza kutoka bara moja hadi jingine.
Rais Trump alifahamishwa juu ya jaribio hilo lililofanywa masaa machache kabla ya Makamu wa Rais Mike Pence kuwasili Korea Kusini, kwa mashauri kuhusiana na Pyongyang na mipango yake ya makombora ya kinyukilia.
No comments:
Post a Comment