Duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge yaanza Ufaransa
Raia wa Ufaransa leo hii wameanza kupiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge nchini humo, huku chama chenye mwaka mmoja tangu kuundwa kwake cha mrengo wa wastani cha rais aliechaguliwa hivi karibuni Emmanuel Macron kikitabiriwa kushinda wingi wa viti bungeni. Uchunguzi wa mwisho wa maoni uliofanyika mara ya mwisho unamweka Macron na chama chake cha "The Republic on the Move," LREM katika asilimia 29 hadi 31.3 katika duru hii. Mpinzani wake wa karibu chama cha mrengo wa kati kulia "Les Republicains" kinaweza kuibuka na asilimia 19 hadi 23. Wakati huohuo chama cha kisoshalisti cha mtangulizi wa Macron, Francois Hollande,kipo katika mashaka ya kuporomoka. Macron ana matumani ya kuibuka na wabunge 577 katika bunge la taifa ili aweze kuidhinisha serikali yake, inayoongozwa na Waziri Mkuu Edouard Philippe.
No comments:
Post a Comment