Mtoto wa miaka 8 aendesha gari kununua chakula duka la McDonald's
Mtoto mmoja mvulana mwenye umri wa 
miaka minane katika jimbo la Ohio, aliendesha gari akiwa na dadake mdogo
 hadi  duka la McDolad's baada ya kujifunza kuendesha gari kupitia 
mtandao wa YouTube.
Jarida na Morning Journal la Ohio lilisema 
kuwa polisi walipigiwa simu kutoka kwa wenyeji kuhusu mtoto ambaye 
alikuwa akindesha gari mjini.Wafanyakazi katika mkahawa wa McDolad's walidhani kuwa ulikuwa ni mchezo wa kuigiza wakati mtoto huyo alisimamisha gari kwenye dirisha kununua chakula.
Mtoto huyo alifuata shera zote za barabara, mtu mmoja aliyeshuhudia alisema.
"Hakugonga chochote njiani, polisi Jacob Koeher kutoka kijiji cha East Palestine alisema

No comments:
Post a Comment